Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 06, 2025 Local time: 23:27

Watu 5 wauawa katika shambulizi la droni kwenye mpaka wa Ukraine na Russia


Uchunguzi katika eneo lililoshambuliwa kwa ndege isiyo na rubani nchini Ukraine.
Uchunguzi katika eneo lililoshambuliwa kwa ndege isiyo na rubani nchini Ukraine.

Shambulizi la ndege isiyo na rubani za Ukraine lililolenga nyumba moja katika kijiji kilicho kwenye mpaka na Russia liliua watu watano, wakiwemo watoto wawili, gavana wa eneo hilo alisema Jumamosi.

Droni hiyo iligonga nyumba katika kijiji kidogo cha Gorodishche, katika eneo la Kursk nchini Russia, mita chache tu kutoka kwenye mpaka na Ukraine.

"Kwa huzuni mkubwa, watu watano waliuawa ... ikiwa ni pamoja na watoto wawili wadogo. Wanafamilia wengine wawili wako katika hali mbaya," gavana wa Kursk Alexei Smirnov alisema katika ujumbe kwenye mtandao wa Telegram.

Shambulio hilo lilikuwa la ndege isiyo na rubani ya "inayofanana na helikopta", aliongeza, akimaanisha drone yenye kifaa kidogo ambacho kinaweza kubebea maguruneti au vilipuzi vingine vya kufanya mashambulizi.

Pande zote mbili zimetumia ndege zisizo na rubani, ikijumuisha vyombo vikubwa vya kujilipua, vyenye uwezo wa kusafiri hadi mamia ya kilomita, kwa muda mrefu, katika mzozo huo ulioanza Februari 2022.

Ukraine imezidisha mashambulizi yake katika eneo la Russia mwaka huu, ikilenga vituo vilwili nishati ambavyo inasema vinawezesha jeshi la Russia kutekeleza mashambuzlizi, pamoja na miji na vijiji katika upande wa pili wa mpaka.

Forum

XS
SM
MD
LG