Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:05

14 wafariki katika ajali ya barabarani Nigeria


Kano, Nigeria.
Kano, Nigeria.

Watu 14 waliuawa wakati lori lilipogonga waumini wa Kiislamu nje ya mji wa Kano, kaskazini mwa Nigeria, mamlaka ya usalama barabarani nchini humo ilisema.

Lori lililokuwa limebeba mizigo lilipoteza udhibiti na kuwagonga waumini waliokuwa wakitoka msikitini muda mfupi baada ya sala ya Ijumaa katika kijiji cha Imawa, kilomita 30 nje ya mjui wa Kano, mamlaka ya serikali kuu ya Usalama Barabarani ilisema katika taarifa yake.

Ajali ni za barabarani na jambo la kawaida katika barabara za Nigeria ambazo hazijatunzwa vizuri kutokana na mwendo kasi na kutozingatia sheria za barabarani.

Kwa mujibu wa tume ya usalama barabarani, zaidi ya watu 5,000 walifariki katika ajali za barabarani mwaka 2023, huku vifo 6,500 vikiripotiwamwaka uliopita.

Hata hivyo shirika la Afya Duniani lilikadiria katika ripoti ya mwaka jana kwamba vifo vya kila mwaka vinavyohusishwa na ajali za barabarani nchini Nigeria kwa kweli ni karibu 40,000, na nyingi zake hazijaripotiwa kwa mamlaka.

Forum

XS
SM
MD
LG