Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Julai 03, 2024 Local time: 22:02

Wamalawi waomboleza kifo cha aliyekuwa Makamu wa Rais


Wafuasi wa chama cha United Transformation Movement wakiomboleza kifo cha mwanzilishi na rais wa chama hicho Saulos Klaus Chilima. Picha na AFP
Wafuasi wa chama cha United Transformation Movement wakiomboleza kifo cha mwanzilishi na rais wa chama hicho Saulos Klaus Chilima. Picha na AFP

Raia wa Malawi walikusanyika kuomboleza kifo cha aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo Saulos Klaus Chilima huku kukiwa na ulinzi mkali siku ya Jumatatu.

siku moja baada ya watu kutoka kwenye kijiji chake kuanzisha maandamano kuhusiana na majibu ya serikali kwa ajali ya ndege iliyomuua makamu huyo wa rais na watu wengine wanane.

Chilima mwenye umri wa mika 51, amezikwa katika kijiji chake cha Nsipe kilichopo katika wilaya ya Ntcheu, kiasi cha kilometa 160 Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Lilongwe.

Jioni kabla ya siku hiyo, umati – uliosema kuwa maafisa hawakuharakisha kufanya msako na uokoaji wakati ndege ya kijeshi ilipopotea - waliziba barabara na kutupa mawe kwa msafara wa magari ya mazishi yalipowasili.

Gari iliyokuwa katika msafara ulioubeba mwili wa aliyekuwa makamu wa rais wa Malawi uligonga waombolezaji waliokuwa kijijini siku ya Jumapili usiku na kuua watu wanne na kujeruhi 12, polisi wamesema.

“Kutokana na ajali hiyo wanawake wawili na wanaume wawili watembea kwa miguu wamepata majeraha mabaya kichwani na kuvunjika sehemu kadhaa na kufariki wakati wakipatiwa matibabu” taarifa ya polisi ilisema.

Forum

XS
SM
MD
LG