Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 22:14

Wairani wazungumzia kuungana kufuatia kifo cha rais wao


Waombolezaji wakihudhuria msafara wa mazishi ya Rais wa Iran Ebrahim Raisi katika Madhehebu ya Waislamu wa Shiite huko Qom, Mei 21, 2024. Picha na HAMID ABEDI / IRNA / AFP.
Waombolezaji wakihudhuria msafara wa mazishi ya Rais wa Iran Ebrahim Raisi katika Madhehebu ya Waislamu wa Shiite huko Qom, Mei 21, 2024. Picha na HAMID ABEDI / IRNA / AFP.

Wakaazi wa Tehran siku ya Jumanne walizungumzia kuungana pamoja kufuatia kifo cha rais wa Iran Ebrahim Raisi aliyefariki katika ajali ya helikopta.

Maelfu ya watu walikusanyika Jumanne katika ibada ya mazishi ua kiongozi huyo pamoja na washuri wake saba walofariki kwenye ajali hiyo.

Watu walipeperusha bendera ya Iran na mabango yaliyoonyesha picha ya rais huyo wa Iran.

Waombolezaji walikusanyika kwenye uwanja wa kati wa mji wa Tabriz kaskazini magharibi mwa nchi na kutembea pembeni ya lori lililobeba jeneza la kiongozi huyo na maafisa wengine.

Tabriz ni mji ambao Raisi alikuwa akielekea wakati helikopta ilipoanguka siku ya Jumapili.

Raisi pamoja na waziri wake wa mambo ya nje Hossein Amir- Abdollahian na watu wengine sita walikufa wakati helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka wakati kukiwa na hali ya hewa mbaya siku ya Jumapili.

Ibada za mazishi yake na watu kuaga mwili wake zinaanza hii leo na kuendelea hadi alhamisi kupitia miji ya Tabriz, QOM, Tehran na Birjand hadi mji alikotokea Masshad ambako maziko yake yatafanyika na kuzikwa kwenye madhabahu ya Imam Reza kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran.

Forum

XS
SM
MD
LG