Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 12:08

Serikali kadhaa zatoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Rais wa Iran Ebrahim Raisi


IRAN-SECURITY/PRESIDENT-RAISI
IRAN-SECURITY/PRESIDENT-RAISI

Pakistan imetangaza siku moja ya maombolezo, nayo Lebanon imetangaza siku tatu za maombolezo, huku serikali kadhaa zikitoa salamu za rambirambi kwa Iran baada ya kifo cha Rais Ebrahim Raisi na waziri wa mambo ya nje Hossein Amirabdollahian katika ajali ya helikopta.

Viongozi hao wa Iran walikuwa wanasafiri kurudi nyumbani kutoka kwenye mpaka wa Iran na Azerbaijan wakati helikopta hiyo ilipoanguka jana Jumapili.

Rais wa Russia Vladimir Putin amempongeza Raisi kama “mwanasiasa mashuhuri”.

Rais wa China Xi Jinping amekitaja kifo cha Raisi kuwa cha “kusikitisha” na kusema “Wachina wamepoteza rafiki mzuri,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje alisema.

Rais wa Syria Bashar al-Assad alionyesha mshikamano wake na Iran, na kusema alifanya kazi na Raisi “kuhakikisha kuwa uhusiano wa kimkakati kati ya Syria na Iran unastawi kila mara.”

Rais wa Misri Abdel Fattah El-Sisi alionyesha mshikamano wa Misri na “uongozi na wananchi wa Iran katika msiba huo mkubwa.”

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amemtaja Raisi kama “ mwenza wa thamani na ndugu.”

Forum

XS
SM
MD
LG