Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 21:31

Viongozi wa dunia wamkumbuka Rais wa Iran Ebrahim Raisi


Mishumaa imewashwa kuomboleza kifo cha rais wa Iran Ebrahim Raisi na timu yake nje ya ubalozi wa Iran ulioko Baghdad, Mei 20, 2024. Picha na REUTERS/Thaier Al-Sudani.
Mishumaa imewashwa kuomboleza kifo cha rais wa Iran Ebrahim Raisi na timu yake nje ya ubalozi wa Iran ulioko Baghdad, Mei 20, 2024. Picha na REUTERS/Thaier Al-Sudani.

Viongozi wa dunia walokua wakihuddhuria mikutano mbali mbali wametoa heshima zao Jumatatu kwa kunyamaza kimya kwa dakika moja kumkumbuka rais wa Iran na washauri wake wa karibu waliofariki katika ajali ya helikopta siku ya Jumapili.

Kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wajumbe walinyamaza kimya kabla ya kuanza kikao cha asubuhi kama ilivyotokea mjini Doha, Qatar kwenye mkutano wa Jopo na Usalama na kwenye makao makuu ya Idara ya Atomiki ya Umoja wa Mataifa mjini Vienna.

Rais wa mwezi huu wa Mei wa baraza hilo Balozi wa Msumbuiji Pedro Comissario Afonso, aliwaomba ajumbe kusimama kimya “kukumbuka Raisi na ujumbe wake waliofariki katika ajali" hiyo.

Viongozi mbali mbali wa duniani waendelea pia kutoa salama za rambirambi kutokana na kifo hicho wakiwemo viongozi wa Russia na China wakimtaja kiongozi huyo mhafidhina mwenye itikadi kali, kuwa ni rafiki wa karibu.

Rais wa China Xi Jimping amesema kifo chake cha kusikitisha ni hasara kubwa kwa watu wa Iran na watu wa China, wamepoteza rafiki mzuri.

Rais wa Russia Vladmir Putin alimsifu Raisi kama mwanasiasa mashuhuri na kusema kuwa kifo chake ni hasara isiyoweza kuzibwa.

Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michael alisema katika taarifa kuwa umoja wa ulaya umetuma salam za rambirambi, na pole nyingi ziwafikie familia yake.

Miongoni mwa viongozi wa Afrika waliotuma rambirambi zao ni pamoja na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani, Rais William Ruto wa Kenya na mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Faki Mahamet.

Serikali ya Iran, imetangaza siku tano za maombolezo kufuatia ajali hiyo iliyosababisha vile vile kifo cha Waziri wa mambo ya Nje Hossein Amir Abdollahian.

Baadhi ya taarifa hizi zinatoka katika Shirika la habari la AFP na Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG