Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 02:38

Ajali ya treni yaua watu 15 India


Wafanyakazi wa shirika la reli wakijaribu kufanya marekebisho katika eneo la ajali huko Nirmaljote, Picha na DIBYANGSHU SARKAR / AFP
Wafanyakazi wa shirika la reli wakijaribu kufanya marekebisho katika eneo la ajali huko Nirmaljote, Picha na DIBYANGSHU SARKAR / AFP

Treni ya mizigo iligonga sehemu ya nyuma ya treni ya abiria iliyokua imesimama katika jimbo la West Bengal nchini India Jumatatu, na kuua takriban watu 15 na kujeruhi kadhaa, kwa mujibu wa maafisa wa polisi wakati madereva wa treni hizo wakilaumiwa.

Kanda za video zilionyesha wanajeshi wa Kikosi cha Kitaifa cha Kukabiliana na Maafa (NDRF) wakifanya shughuli za uokoaji karibu na sehemu za treni zilizoharibika.

Akizungumza na waandishi wa Habari, Jaya Varma Sinha, mkuu wa bodi ya reli inayoendesha mtandao huo nchini kote, alisema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa treni hiyo ya mizigo kupuuza ishara na kugonga sehemu ya nyuma ya treni ya mwendokasi.

Treni hiyo ya mizigo iligonga Express ya Kanchanjunga iliyokuwa ikisafiri kuelekea Kolkata, mji mkuu wa West Bengal, kutoka jimbo la kaskazini mashariki la Tripura, ikiendesha mabehewa matatu ya treni ya abiria kutoka kwenye reli.

Forum

XS
SM
MD
LG