Mwanasiasa huyo ameahidi kuimarisha uwekezaji katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi inapojiandaa kuanza uzalishaji wa gesi asilia.
Ghazouani, mwenye umri wa miaka 67, ambaye zamani alikuwa afisa mwandamizi wa kijeshi, ameahidi sera rafiki kwa wawekezaji ili kuchochea ukuaji wa bidhaa katika nchi hiyo yenye watu milioni 5, ambao wengi wao wanaishi katika umaskini licha ya utajiri wake wa mafuta na madini.
"Neno la mwisho ni la wapiga kura wa Mauritania. Ninajitolea kuheshimu chaguo lao," Ghazouani alisema baada ya kupiga kura katika mji mkuu.
Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi saa za huko, na zoezi hilo lilitarajiwa kumalizika saa moja jioni, huku matokeo ya awali yakitarajiwa kuanzia Jumapili.
Ghazouani alichaguliwa kwa muhula wa kwanza mnamo 2019, na anakabiliana na wapinzani sita, kati yao akiwa ni mwanaharakati wa kupinga utumwa, Biram Dah Abeid, ambaye aliibuka wa pili katika uchaguzi wa mwaka 2019 kwa kupata zaidi ya asili mia 18 ya kura.
Forum