Rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani atakabiliana na wapinzani sita katika uchaguzi wa rais wa nchi hiyo Juni 29, kulingana na orodha ya mwisho iliyowasilishwa Jumatatu na baraza la katiba.
Ghazouani mwenye miaka 67 anapigiwa upatu kushinda muhula wa pili kama kiongozi wa taifa hilo lenye watu milioni 4.5 ambalo liko katika eneo la kimkakati, kati ya kaskazini na kusini mwa jangwa la Sahara.
Baraza hilo halikumkubali rais wa zamani kugombea, Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye yuko gerezani kwa ubadhirifu, jambo ambalo amekuwa akilikanusha siku zote.
Aziz aliruhusiwa kutoka gerezani wiki iliyopita ili kuwasilisha fomu yake ya kugombea urais katika baraza la katiba, lakini ilikataliwa kwa kuwa na idadi ndogo ya wadhamini, kilisema chanzo kilicho karibu na baraza hilo.
Miongoni mwa wagombea wanaotarajiwa katika uchaguzi wa Juni, ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Kiislamu, Hamadi Ould Sid' El Moctar, na mwanaharakati wa haki za binadamu Biram Ould Dah Ould Abeid, ambaye alishika nafasi ya pili nyuma ya Ghazouani katika uchaguzi wa 2019.
Mauritania ilikumbwa na msururu wa mapinduzi kuanzia mwaka 1978 hadi 2008, kabla ya uchaguzi wa mwaka 2019, kuwa wa kwanza kati ya marais wawili waliochaguliwa.
Huku ujihadi ukiwa umesambaa, kwengineko katika eneo la Sahel, hasa katika nchi jirani ya Mali, Mauritania hazijashuhudia shambulio lolote tangu mwaka 2011.
Forum