Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 28, 2024 Local time: 01:36

Watoto 3,000 walijaribu kuingia Marekani kupitia Mexico


Wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali wanaojaribu kuingia Marekani wakiwa Mexico City Juni 6, 2024. PIcha na Yuri CORTEZ / AFP.
Wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali wanaojaribu kuingia Marekani wakiwa Mexico City Juni 6, 2024. PIcha na Yuri CORTEZ / AFP.

Takriban watu milioni 1.39 kutoka nchi 177 walisafiri kupitia Mexico hadi sasa mwaka huu wakijaribu kuingia Marekani bila kuwa na stakabadhi muhimu, kwa mujibu wa serikali ya Mexico.

Taasisi ya Kitaifa ya Uhamiaji ikitoa takwimu za Januari hadi mwisho wa Mei, ilisema idadi kubwa walikuwa wanaume na wanawake waliokuwa wakisafiri peke yao, wakati idadi ya watoto 3,000 walikuwa waliokuwa peke yao.

Idadi hiyo ya nchi 177 zilizotajwa ni karibu sawa na watu kutoka sehemu zote za dunia kwani Umoja wa Mataifa una nchi wanachama 193.

Idadi kubwa zaidi ya wahamiaji wanaotarajiwa kuwa karibu 380,000 walitoka Venezuela, ambayo imekuwa ikikabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi, ikifuatiwa na Guatemala, Honduras, Ecuador na Haiti, ambazo zote zimeathiriwa sana na magenge na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Wahamiaji wengine wanaojaribu kufanya safari za hatari kupitia Mexico kutafuta maisha bora nchini Marekani walitoka mbali kama China, India, Mauritania na Angola, taasisi hiyo ilisema.

Forum

XS
SM
MD
LG