Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 08:22

Biden apitisha amri ya kiutendaji kukabiliana na uhamiaji haramu


Rais Joe Biden akizungumza kuhusu amri ya kiutendaji ya kukabiliana na uhamiaji haramu, Juni 4, 2024.
Rais Joe Biden akizungumza kuhusu amri ya kiutendaji ya kukabiliana na uhamiaji haramu, Juni 4, 2024.

Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne ametangaza amri ya kiutendaji ambayo itazuia kwa muda haki ya kupewa hifadhi kwenye mpaka kati ya Marekani na Mexico muda wowote idadi ya wahamiaji wanaovuka mpaka kinyume cha sheria au bila idhini itafikia wastani wa kila siku wa 2,500.

Amri ya kiutendaji ya Biden inasema wale wanaovuka mpaka kinyume cha sheria kuingia nchini hawatastahiki kupata hifadhi ikiwa tu kuna sababu za msingi kwa nini wanapaswa kuruhusiwa kukaa Marekani.

“Hatua hizi pekee hazitaboresha mfumo wetu wa uhamiaji, lakini zinaweza kusaidia kupata makubaliano kwa kukabiliana vyema na changamoto hii ngumu,” Biden amesema katika hotuba yake kwenye White House.

Kulingana na maafisa wa Marekani, hatua hizo za muda kuhusu kupewa hifadhi zitaanza kutekelezwa wakati idadi ya wastani ya wanaovuka mpaka kila siku itazidi 2,500, na zitasimamishwa idadi hiyo ikishuka chini ya 1,500.

Hatua hizo zinaanza kutekelezwa mara moja.

Forum

XS
SM
MD
LG