Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 08, 2025 Local time: 22:49

Rais wa Mauritania anatoa wito kwa nchi za Afrika magharibi kuungana pamoja


Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani akiwa mjini Nouakchott, Mauritania.
Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani akiwa mjini Nouakchott, Mauritania.

Eneo hilo lazima litengeneze utashi wa pamoja wa kisiasa kuweza kupambana na ukosefu wa usalama, Ghazouani aliiambia AFP

Rais wa Mauritania Mohamed Ould Cheikh El Ghazouani ametoa wito kwa nchi za Afrika Magharibi kuungana pamoja katika kukabiliana na jihadi, katika mahojiano na shirika la habari la AFP kabla ya uchaguzi wa rais nchini humo.

Eneo hilo lazima litengeneze utashi wa pamoja wa kisiasa ili kuweza kupambana na ukosefu wa usalama, Ghazouani aliliambia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa, wakati wa kampeni kuelekea uchaguzi wa Juni 29. Mimi sio mmoja wa wale wanaofikiri leo kwamba nchi zinaweza kukabiliwa na tishio kama ugaidi.

Mkuu huyo wa zamani wa jeshi na waziri wa ulinzi mwenye umri wa miaka 67 anatazamiwa kuwania muhula wa pili kama kiongozi wa taifa hilo lenye watu milioni 4.5 ambalo liko kimkakati kati ya kaskazini na kusini mwa jangwa la Sahara.

Ameliambia shirika la habari la AFP kwamba hali ya usalama katika eneo hilo dogo sio nzuri kabisa na imekuwa mbaya.

Forum

XS
SM
MD
LG