Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:46

DRC yataka Rwanda iwekewe vikwazo


Wacongo wakivikimbia vijiji vyao kufuatia mapambano kati ya majeshi ya serikali na kundi la M32 huko Kivu Kaskazini Februari 7, 2024. Picha na REUTERS/Arlette Bashiz
Wacongo wakivikimbia vijiji vyao kufuatia mapambano kati ya majeshi ya serikali na kundi la M32 huko Kivu Kaskazini Februari 7, 2024. Picha na REUTERS/Arlette Bashiz

Waziri mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Judith Suminwa Tuluka amesema kwamba serikali ya Kinshasa haitaki mazungumzo na Rwanda, kwa sababu inaituhumu kuwasaidia waasi wa kundi la M23 huko mashariki ya nchi yake.

Alipoitembelea kambi ya wakimbizi karibu na Goma siku ya Alhamis, Tuluka ametoa wito kwa washirika wakuu wa Congo kuchukua hatua kali na vikwazo dhidi ya Kigali.

Hata hivyo siku ya Alhamisi rais wa Angola Joao Lourenco akiwa katika ziara huko Ivory Coast amesema kwamba mazungumzo yananedelea katika kiwango cha mawaziri kwa lengo la kuwaleta pamoja viongozi wa Rwanda na DRC kwa haraka iwezekanavyo ili kukubaliana juu ya kupatikana amani ya kudumu Mashariki ya Congo.

Angola imekua ikijaribu kupatanisha nchi hizo mbili kutokana na ugomvi katika jimbo la kivu ya Kaskazini ambako waasi wa M23 wanadaiwa kuungwa mkono na Rwanda wamekua wakipigana na jeshi la serikali tangu mwishoni mwa 2021.

Forum

XS
SM
MD
LG