Mkurugenzi Mkuu huyo amesema kwamba shirika lake liko tayari kusaidia miradi mikubwa ya maendeleo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Amesema ili mataifa haya yaweze kufanikiwa kuna umuhimu wa kuandaa miradi mizuri ambayo inaweza kupata ufadhili hasa kwa kuzingatia kuwa pesa iliyopo haitoshi.