Wakopeshaji wa kimataifa walisema, kwa uzalishaji wa kimataifa,( pato la jumla la taifa) makadirio ya ukuaji uchumi, hata hivyo bado yako chini ya wastani wa kihistoria kwa asilimia 3.8, uliorekodiwa kati ya mwaka 2000 na 2019, hali hiyo ikichangiwa na vita virefu nchini Ukraine, kabla ya kuimarika kufikia asilimia 3.1 mwaka 2024.
“Mtazamo si mbaya sana kuliko ilivyokuwa katika utabiri wetu wa Oktoba na unaweza kuwakilisha hatua ya mabadiliko, kwa kiwango cha chini kabisa cha ukuaji wa uchumi na kupungua kwa mfumuko wa bei,” Mchumi mkuu wa IMF Pierre-Olivier Gourinchas alisema katika mkutano na waandishi wa habari Jumanne.
Katika ripoti yake ya World Economic Outlook iliyotolewa Oktoba mwaka jana, IMF ilitabiri uchumi wa dunia utashuka hadi asilimia 2.7 ya kiwango cha ukuaji wake kutoka asilimia 3.2 ilivyotarajiwa kwa 2022, kutokana na kuendelea kwa vita nchini Ukraine, kuongezeka mfumuko wa bei na kupungua kwa shughuli za kiuchumi nchini China kufuatia sheria za kudhitibi Covid 19.
Lakini wakati China ikifungua tena uchumi wake kwa wafanyabiashara wa ndani na nje , IMF imesema katika ripoti mpya (WEO) iliyotolewa Jumanne ilitarajia kuwa mfumo wa usambazaji wa bidhaa hautayumba sana mwaka huu wa 2023, uzalishaji utaongezeka na mahitaji yataongezeka na kupelekea ukuaji wa pato la taifa kuliko ilivyotarajiwa awali.
Chanzo cha habari hii ni gazeti la "The East African" linalochapishwa Kenya.