Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 03:51

2023 utakuwa mwaka mgumu kwa uchumi wa dunia


Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva
Mkurugenzi mkuu wa IMF Kristalina Georgieva

Kwa sehemu kubwa ya uchumi wa dunia, 2023 utakuwa mwaka mgumu kwa kiuchumi.

Hii inatokana na vichocheo vikuu vya ukuaji wa uchumi kimataifa yaani Marekani, Ulaya na China, zinakabiliwa na kudhoofu amesema mkuu wa shirika la kimataifa la fedha (IMF) Jumapili.

Mwaka mpya utakuwa mgumu zaidi kuliko uliopita amesema mkurugenzi mkuu wa IMF, Kristalina Georgieva, kwenye kituo cha televisheni ya CBS katika kipindi cha Face the Nation.

Amesema sababu kubwa ni mataifa matatu yenye uchumi mkubwa Marekani, China na yale ya Umoja wa Ulaya kwa pamoja yanakabiliwa na kasi ndogo ya ukuaji uchumi.

Hapo Oktoba, IMF ilisimamisha ubashiri wake wa ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka 2023.

Uchumi ulionyesha kuendelea kudorora kutokana na vita vya Ukraine pamoja na shinikizo la mfumuko wa bei na viwango vya juu vya riba vilivyowekwa na benki kuu kama vile Benki Kuu ya Marekani inayolenga kuondoa msukumo wa mfumuko wa bei.

XS
SM
MD
LG