Ziara ya Pompeo Saudia ni sisitizo la Marekani kuendelea kuihami

Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo, kulia mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa King Khalid, Riyadh, Jumatano, Feb. 19, 2020. (Andrew Caballero-Reynolds/Pool Photo via AP)

Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani katika Kituo cha Kijeshi cha Ulinzi wa Anga cha Prince Sultan (PSAB) na kituo cha kujihami cha Marekani cha Patriot battery inasisitiza mahusiano ya kiusalama ya muda mrefu kati ya Marekani na Saudi Arabia.

Pia ziara hii ni fursa kwa Marekani kuendeleza nia yake ya kusimama na Saudi Arabia dhidi ya tabia hatarishi ya Iran.

Kutembelea kwa Waziri huyo ni umuhimu endelevu unaoweka shinikizo la juu kabisa dhidi ya Iran na kusisitiza ahadi ya Marekani katika kuimarisha usalama wa nchi za Ghuba na utulivu wa eneo la Mashariki ya Kati.

Shambulizi lililofanywa na Iran Septemba 14, 2019 linasisitiza tishio linaloendelea la harakati hatarishi za Iran zinazokabili eneo na tishio la usalama wa dunia na pia masoko ya nishati ya dunia.

Katika kujibu mashambulizi na kwa ombi la Saudi Arabia, Marekani imepeleka mfumo wa kuzuia mashambulizi ya makombora, na ndege za vita katika harakati za kuimarisha ulinzi kuzuia na kulinda nchi ya Saudi Arabia na mashambulizi ya siku zijazo.

Kuwepo kwa ulinzi huu unaimarisha ulinzi wa kijeshi wa Saudi Arabia wenye kuunganisha mifumo ya ulinzi wa angani na makombora ya kuihami miundombinu muhimu ya kijeshi na kiraia.

Marekani kuweka ulinzi huko PSAB ni ishara tosha ya kuwahakikishia wananchi na uongozi wa Saudi Arabia kuwa Marekani inasimama nao wakati wanakabiliwa na vitisho hivi kutoka Iran.