Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 01:08

Pompeo : Wawekezaji wa Marekani wanatoa fursa kwa wananchi wa Angola


Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo (kushoto) akiwa na Rais wa Angola João Lourenço, Jumatatu Februari 17, 2020.(Andrew Caballero-Reynolds/Pool via AP)
Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo (kushoto) akiwa na Rais wa Angola João Lourenço, Jumatatu Februari 17, 2020.(Andrew Caballero-Reynolds/Pool via AP)

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo amekutana na Rais wa Angola Joao Lourenco mjini Luanda Jumatatu, mazungumzo yao yakiangaza juu ya kuboresha ushirikiano wa kiuchumi na kuwasaidia wananchi wa Angola kupiga vita ufisadi.

Lourence alichaguliwa kuwa rais mwaka 2017 wakati Rais wa zamani Jose Eduardo dos Santos alipoachia madaraka baada ya kutawala nchi hiyo kwa miongo mine.

Lourenco amewashangaza wengi kwa utawala wake kuonekana ukipambana na ufisadi kwa nguvu zote.

Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Luanda, Waziri wa Mambo ya Nje Manuel Augosto amesema “anataka kuamini kuwa ujio wa Pompeo ni dalili ya Rais Donald Trump kuunga mkono nchi hiyo,” na ana matumaini ni mwanzo mpya, uhusiano mpya kamili kati ya nchi hizo mbili.

Pompeo amesema hakuweza kujibu swali juu ya lini Trump angeweza kufanya ziara Angola, akisema rais ana shughuli nyingi, hususan katika mwaka wa uchaguzi.

Alipoulizwa kuhusu ushindani uliopo kati ya Marekani na China nchini Angola na maeneo mengine Afrika, Pompeo amesema atawaachia wengine kufanya tathmini jinsi mbinu za Marekani zinavyo tofautiana na China kibiashara, akiongeza, “Tunapokuja nchini kwenu, tunawaajiri wananchi wa Angola.”

Pompeo amemwambia Augusto kuwa ziara yake imekuja wakati muhimu katika historia ya Angola kwa sababu biashara, asasi za kiraia na wananchi wa Angola wako tayari kwa mabadiliko.

Pompeo alisema yeye na viongozi wa Angola walizungumza kwanza jinsi ya kushughulikia zaidi masuala ya ufisadi ambayo yamelikwamisha taifa kwa kipindi kirefu, na kumpongeza Lourenco kwa juhudi zake.

“Amewadhibiti watendaji wabaya. Ni matumaini yangu ataendelea kuwakomboa wananchi wa Angola kutokana na ufisadi,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alisema.

Pompeo pia amegusia mafanikio ya programu za afya zinazosaidiwa na Marekani, ikiwemo juhudi za kupambana na ukimwi, PEPFAR na mradi wa malaria. Amesema idadi ya walioathirika na malaria Angola imepungua kwa asilimia 50 katika miaka ya karibuni.

Pompeo aliwasili Angola jioni Jumapili baada ya ziara yenye tija huko Senegal, ambako alishuhudia kusainiwa kwa hati tano za maelewano katika ushirikiano wa sekta binafsi kati ya makampuni ya Senegal na Marekani.

XS
SM
MD
LG