Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:31

Nzige : Uganda yawekwa katika tahadhari ya upungufu wa chakula


Kundi kubwa la nzige likiwa katika kijiji cha Nakwamuru, Kaunti Samburu, Kenya Januari 16, 2020. REUTERS/Njeri Mwangi/File Photo
Kundi kubwa la nzige likiwa katika kijiji cha Nakwamuru, Kaunti Samburu, Kenya Januari 16, 2020. REUTERS/Njeri Mwangi/File Photo

Uganda imewekwa katika hali ya tahadhari ya upungufu wa chakula wakati nzige kutoka jangwani wakiendelea kushambulia wilaya mbalimbali nchini humo.

Wizara ya Kilimo imesema vikundi vipya viwili vya nzige vimeingia Uganda kutoka Kenya, Jumatano.

Maafisa wamewataka wakulima kuhifadhi chakula na majani kwa ajili ya wanyama wakijiandaa na uharibifu unaotokana na nzige.

Nzige tayari wameangamiza mamilioni ya hekta za mimea katika Pembe ya Afrika.

Mkazi kutoka Wilaya ya Kitgum, Uganda Ocan Acaa (81) hawezi kusahau namna walivyokumbwa na njaa baada ya nzige kuvamia wilaya yake miaka ya 1940 na 1950.

Nakumbuka katika miaka ya 40 hiyo ndio ilikuwa mara ya kwanza nzige kuvamia wakitokea Kitgum na nilishuhudia mwenyewe. Pia niliwala nzige hao nikiwa kijana mdogo.

Kwa hiyo nzige wakubwa walipoondoka walifuatiwa na nzige wadogo. Hao ndio walikula kila kitu mpaka ukawa huwezi kuona jani la kijani hata moja.

Uganda hivi sasa inajitayarisha kukabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula iwapo nzige hao wa jangwani hawatadhibitiwa katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

Nzige hao walioingia Uganda kupitia Wilaya ya Amudat nchini Kenya wakati wa wikiendi wameonekana kuanzia wakati huo katika wilaya nyingine takriban nane.

Nzige hao wanasemekana kuwa wanazunguka katika vikundi vidogo vidogo vya nzige 50,000 na hawajasababisha madhara yoyote hadi sasa.

Lakini, maafisa wa kilimo Uganda wanaeleza kuwa madhara zaidi yanatarajiwa baadae wakati nzige hao wakianza kuzaana.

XS
SM
MD
LG