Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:17

Marekani kusaidia mageuzi ya kisiasa Ethopia


Waziri mkuu wa Ethopia Abiy Ahmed akutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani ofisini mwake Addis Ababa.
Waziri mkuu wa Ethopia Abiy Ahmed akutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani ofisini mwake Addis Ababa.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo ameahidi kusaidia mpango mkubwa wa mageuzi ya kisiasa nchini Ethopia baada ya kukutana na waziri mkuu Abiy Ahmed mjini Addis Ababa Juamnne asubuhi.

Akiwa katika kituo chake cha mwisho cha ziara ya mataifa matatu ya Afrika,mwanadiplomasia mkuu wa Marekani amesema nchi yake itaimarisha ushirikaino wa biashara na nchi za Afrika na juhudi za kupambana na rushwa.

Pompeo aliyewasili Addis Ababa Jumatatu usiku akitokea Luanda, Angola alikutana na mshindi wa tunzo ya Nobel ya Amani, Bw. Ahmed na kujadili mageuzi ya kisiasa yanayofanyika nchini mwake na namna Marekani itakavyoweza kusaidia kifedha juhudi hizo.

Akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano wao, Pompeo alitangaza kwamba Marekani itatoa msaada ziada wa dola milioni 8 kuasaidia katika juhudi za kupambana na uvamizi wa nzige katika pembe na mashariki ya Afrika.

Mzozo kati ya Ethopia na Misri utachukua muda kutanzuliwa

Ofisii ya waziri mkuu wa Ethopia, imeeleza kwamba mwanadiplomasia mkuu wa Marekani alijadili pia juu ya masuala ya kikanda ikiwa ni pamoja na mvutano kati ya Ethopia na Misri juu ya ujenzi wa bwawa la Grand ethopia Renaissance Dam, kwenye mto wa Blue Nile.

Akizungumza na waandishi habari Pompeo amesema itachukua miezi kadhaa kabla ya kutanzua ugomvi kati ya Ethopia na Misri juu ya bwawa hilo.

Pompeo alikutana pia na rais Sahle-Work Zwewde na kujadili juu ya matayarisho ya uchaguzi mkuu mwezi Ogusti mwaka huu na juhudi za kupanua uhuru wa kujieleza na kukutana huko Ethopia.

Rais Sahle-Work wa Ethopia akizungumza na Mike Pompeo mjini Addis Ababa.
Rais Sahle-Work wa Ethopia akizungumza na Mike Pompeo mjini Addis Ababa.

Ethopia taifa la pili la afrika lenye wakazi wengi likiwa na wakazi milioni 100, na mshirika mkuu wa Marekani inashuhudia mageuzi muhimu ya kisiasa yaliyoanzishwa mwaka jana na mshindi wa tunzo ya Nobel.

Lakini changemoto kuu inayo mkabili ni nkutekeleza vilivyo mageuzi hayo ni uchaguzi mkuu ujao ambao ameahidi utakua wa huru na haki.

“Uchaguzi wa huru na haki utadhihirisha kwamba kila mtu anasauti katika manegeuzi haya,” amesema Pompeo.

Akiwa Lunada siku ya Jumatatu Pompeo alimpongeza rais Joao Laurence kwa juhudi zake za kupambana na ulaji rushwa hasa akimfuata miongeni mwa wengine binti yake rais wa zamani Isabel dos Santos kwa ubadhirifu wa mali.

Anasema, “mnamo miaka miwili na nusu madarakani Rais Lorenco amefanya kazi kuba kuhakikisha ulaji rushwa na zingaombwe la zamani.”

Mwanadiplomasia huyo alisema amefurahishwa na juhudi za rais kubinafsisha mashirikas 195 ya umaa, akisema hatua hiyo muhimu itawavutia sana wawekezaji.

XS
SM
MD
LG