Nchi zimetakiwa kufikiria kuwashauri wasafiri kuvaa barakoa wakati wa safari ndefu za ndege ili kupambana na maambukizi ya hivi karibuni ya virusi vya COVID 19 aina ya Omicron kutokana na kusambaa kwake kwa kasi nchini Marekani, maafisa wa Shirika la Afya Duniani wamesema Jumanne.
Kiwango kidogo cha virusi aina ya XBB.1.5 kimegunduliwa katika nchi za Ulaya, na idadi ya maambukizi inaendelea kuongezeka, huku maambukizi yanaongezeka kwa kasi katika sehemu mbalimbali za Marekani, mkurugenzi wa WHO kwa nchi za Ulaya Hans Kluge amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Wasafiri washauriwe kuvaa barakoa katika mazingira ambayo yana hatari kubwa sana kama vile safari za muda mrefu za anga amesema afisa mkuu wa WHO anayeshughulikia masuala ya dharura kwa nchi za Ulaya, Catherine Smallwood, na kuongeza kuwa “hili liwe pendekezo kwa wasafiri wanaowasili kutoka sehemu mbalimbali zenye kiwango kibubwa cha maambukizi ya COVID-19.