China ilipinga masharti mapya ya upimaji wa COVID-19 kwa wasafiri wa China ambayo yamewekwa na nchi kadhaa, ikisema hatua hizo "hazina msingi wa kisayansi".
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Mao Ning aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano kwamba China inaweza kuanzisha "hatua za kukabiliana nazo kwa kuzingatia kanuni ya usawa".
China imeshuhudia ongezeko la maambukizi ya COVID-19, huku serikali nyingine zikiikosoa China kwa kutokuwa wazi kuhusu takwimu zake za maambukizi.
Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Marekani (CDC) kilitangaza wiki iliyopita kwamba abiria wanaotumia usafiri wa anga kutoka China watalazimika kuonyesha kipimo cha COVID-19 chenye kuonyesha majibu sahihi au uthibitisho wa kupona kabla ya kuruhusiwa kupanda ndege. Taarifa ya CDC ilinukuu "ukosefu wa data za kutosha na uwazi kwa magonjwa na virusi aina ya genomic vinavyoripotiwa" kutoka China.
"Takwimu hizi ni muhimu kufuatilia kuongezeka kwa kesi kwa ufanisi na kupunguza nafasi ya kuingia aina tofauti ya virusi vipya” CDC ilisema.