Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:17

Wagonjwa wapya Covid-19 waendelea kumiminika kwenye hospitali za China


Wagonjwa wa Covid kwenye chumba cha dharura katika hospitali moja mjini Shanghai. Januari 5,2023
Wagonjwa wa Covid kwenye chumba cha dharura katika hospitali moja mjini Shanghai. Januari 5,2023

Wagonjwa, wengi wao wazee wako kwenye vitanda vya wagonjwa nje ya wodi za hospitali baadhi wakituwa na mitungi ya Oksijeni na wengine wakiwa wamekaa kwenye  viti vya magurudumu katika mji  mkuu wa China, Beijing kutokana na wimbi jipya la maambukizi ya Covid-19.

Hospitali ya Chuiyangliu mashariki mwa mji huo Alhamisi ilikuwa imefurika wagonjwa wapya huku vitanda vyote vikiwa vimejaa wagonjwa wakati magari ya kubeba wagonjwa yakiendelea kuleta wagonjwa zaidi. Madaktari na wauguzi wameonekana wakijitahidi kuchukua taarifa za wagonjwa wanaowasili, huku wakishughulikia kesi za dharura zaidi.

Wimbi jipya la maambukizi nchini China linahusishwa kutokana na kulegezwa kwa kanuni kali za kuzuia maambukizi mwezi uliopita baada ya shughuli za kawaida kufungwa kwa karibu miaka mitatu. Kufungwa kwa usafiri, biashara pamoja na shule kuliathiri pakubwa uchumi wa taifa na kupelekea maandamano makubwa yanayoweza kulinganishwa na yale yalioshuhudiwa katika miaka ya 80.

Hali hiyo imejitokeza wakati Umoja wa Ulaya ukipendekeza kwamba mataifa wanachama yaweke kanuni za upimaji wa Covid kwa wasafiri wanaotokea China.

XS
SM
MD
LG