Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:25

Ulimwengu waukaribisha mwaka mpya kwa sherehe mbali mbali


Sherehe za mwaka mpya huko Times Square New York. Januari 1, 2023.REUTERS.
Sherehe za mwaka mpya huko Times Square New York. Januari 1, 2023.REUTERS.

Ulimwengu uliukaribisha mwaka mpya kwa sherehe iliyojaa watu huko Times Square New York na fataki zilizotanda anga katika miji mikuu ya Ulaya, huku kukiwa na matarajio ya kumalizika kwa vita nchini Ukraine na kurejea kwa hali ya kawaida ya baada ya COVID-19 huko Asia.

Ulikuwa ni mwaka ulioadhimishwa na mzozo wa Ukraine, matatizo ya kiuchumi na athari za ongezeko la joto duniani. Lakini pia ulikuwa mwaka ambao ulishuhudia Kombe la Dunia la kandanda, mabadiliko ya haraka ya teknolojia, na juhudi za kukabiliana na changamoto za hali ya hewa.

Baada ya mwaka 2023 kusheherekewa barani Asia, Afrika na Ulaya, New York iligonga mwaka mpya kwa mtindo wake wa kawaida huku maelfu ya watu walijipanga kwenye sehemu moja wakati mvua ikiendelea kunyesha huko Times Square, wakisubiri kwa saa kadhaa ili kushuhudia 'mpira' wa aina yake ukishushwa kuhesabu kuingia mwaka mpya.

'Mpira' huo ulikuwa na ukubwa wa futi 12 ulishushwa chini ya nguzo juu ya jengo ya ghorofa 25 ili kuashiria mabadiliko ya kalenda.

Wakati huohuo, mamilioni ya watu walitazama maonyesho ya muziki yaliyoambatana na kuhesabu kuingia mwaka mpya kwenye televisheni wakiwa majumbani mwao duniani kote.

XS
SM
MD
LG