WHO yaonya mataifa 42 ya Afrika kutofikia lengo la chanjo la asilimia 10

Ramani ya Afrika

Ofisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya Afrika imeonya Alhamisi mataifa 42 kati ya 52 ya Afrika hayataweza kufikia shabaha ya chini iliyowekwa kuchanja angalau asilimia 10.

Shabaha hiyo ya chini inazitaka nchi za Afrika kuwapatia chanjo wakazi wake dhidi ya ugonjwa wa Covid 19 kabla ya mwisho wa mwezi Septemba.

Mkurugenzi wa kikanda wa ofisi hiyo Matshidiso Rebecca Moeti akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya janga hilo barani humo amesema hali hiyo inatokana na kutokuwepo na mpango wa kugawanya kwa usawa chanjo.

Moeti anasema idadi ya wagonjwa wa COVID-19 wiliothibitishwa barani Afrika inakaribia milioni 8 wakati idadi ya waliofariki imepindukia 196,000 kufikia jana.

Anasema Kutokana na mataifa Tajiri kuhodhi chanjo nchi za Afrika Kusini ziko nyuma kabisa katika kutoa chanjo ma hivyo idadi ya wagonjwa mahtuti na vifo inazidi kuiongezeka.