Johnson alikuwa anazungumza mjini New York, anakohudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, baada ya mahakama kuu ya Uingereza kwa sauti moja kuamua kwamba hatua yake ya kuahirisha kikao cha Bunge imekwenda kinyume cha sheria na haiwezi kutekelezwa.
Vyama vya upinzani mara moja vimemtaka waziri mkuu ajiuzulu na kikao cha bunge kuitishwa Jumatano.
Mahakimu 11 wa mahakama kuu ya Uingereza kwa sauti moja walisema hatua ya Johnson kumshauri Malkia Elizabeth kuahirisha kikao cha bunge inakwenda kinyume na katiba.
Bunge liliahirishwa na waziri mkuu hapo sep[temba 10 wakati wa majadiliano juu ya pendekezo la Johnson kutaka uchaguzi wa mapema kufanyika kabla ya muda wa Uingereza kujiundowa kutoka umoja wa Ulaya hapo Oktoba 31.
Johnson alitaka kupewa nafasi ya kuiondoa Uingereza kutoka EU hata ikiwa hakuna mkataba ya kuondoka unafikiwa jambo ambalo upinzani umepinga vikali.
Baraza kuu la bunge, lnalofahamika kama House of Commons litakutana tena kesho kufuatoia uwamuzi huo wa mahakama na spika wa baraza hilo John Brecow anasema kitakua kikao cha kawaida bila ya kipindi cha maswala na majibu.
Viongoi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour kimesema kitafikishahoja ya kutokuwa na imani na wazir mkuu, wakisema ametumia vibaya mamlaka yake na kumpotosha Malkia.
Johnson alichukua madaraka baada ya alieymtangulia Theresa May kushindwa mara tatu kulihimiza baraza kuu la bunge kuidhinisha makubaliano yake aliyofikia na wakuu wa EU.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC.