Waziri Mkuu wa Uingereza aendelea na matibabu hospitalini

Waziri Mkuu Boris Johnson

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliyekuwa amepimwa wiki iliyopita na kukutikana na maambukizi ya virusi vya corona, amelazwa hospitali Jumatatu baada ya kupokelewa kwa ajili ya kufanya vipimo zaidi kutokana na homa kali iliyokuwa inaendelea.

Ofisi yake imesema hatua hiyo ni ya kuchukua “tahadhari” na kuwa bado anaendelea kuliongoza taifa la Uingereza.

Wakati huohuo vifo kutokana na virusi vya corona vilivyotokea Jumatatu duniani ni 1,021 kwa mujibu wa taarifa za mtandao wa WorldOMeter. Taarifa hiyo inaonyesha maambukizi duniani yamefikia watu 1,286,294, vifo 70,446 na waliopona ni 271,882 hadi hivi leo.

Uingereza

Uingereza imeibuka kuwa moja ya maeneo yaliyoathirika zaidi katika janga hili, na imeripoti vifo zaidi ya 600 Jumapili.

Maeneo mengine ya Ulaya yameonyesha kuwepo nafuu ya maambukizi na vifo baada ya kuathirika vibaya sana kutokana na virusi hivyo ambavyo vimesababisha serikali mbalimbali kutoa amri ya watu kutotoka majumbani ili kupunguza kuenea kwa maradhi hayo

Itali

Italy, ambayo ina vifo vingi zaidi, imeripoti idadi ndogo ya vifo katika wiki mbili, wakati Uhispania pia imeripoti mtiririko wa hivi karibuni ya ugonjwa huo wa idadi ya chini katika vifo na maambukizi mapya.oss the country to New York, the hardest-hit area in the country.

Marekani

Nchini Marekani, majimbo ya magharibi ya Oregon na Washington yamesema watatuma New York ambako ndio kwenye maambukizi zaidi nchini maelfu ya vifaa vya kusaidia kupumua vinavyo hitajika kwa dharura kote Marekani.

Takriban thuluthi yawatu 9,600 waliokufa kutokana na virusi vya corona nchini Marekani ni wakazi wa New York, ambako hospitali za muda zimejengwa katika viwanja vya mji huo na meli yenye hospitali ya jeshi la majini linasaidia kupunguza mzigo mkubwa wa wagonjwa unaoikabili mifumo ya afya ya mji huo.

Maeneo mengine ya nchi ya Marekani yanaendelea kuonyesha wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya maambukizi, ikiwemo Pennsylvania, Colorado na mji mkuu wa Marekani, Washington, DC ambako imethibitishwa kuwepo watu 1,000 wenye maambukizi.

Korea Kusini

Korea Kusini, moja ya maeneo ya yaliyoathiriwa zaidi wakati wa mlipuko wa maradhi hayo, umeripoti maambukizi mapya 47 Jumatatu, lakini naibu waziri wa afya wa nchi hiyo ametahadharisha juu ya umuhimu wa watu kuendelea kuwa waangalifu na kutotoka majumbani ili kuepusha “mlipuko” wa maambukizi.

Kim Gang-lip amesema takwimu zilizo kusanywa kutoka katika simu aina ya smartphones zinaonyeshawatu wengi wanatoka kwenda kwenye migahawa na viwanjani katika wiki za hivi karibuni.

Japan

Nchini Japan maambukizi 3,600 yameripotiwa hadi hivi sasa, lakini wasiwasi unaongezeka kutokana na baadhi ya maeneo ya nchi hiyo, ikiwemo Tokyo, idadi ya maambukizi imekuwa ikiongezeka kwa kasi kubwa.

Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe amesema serikali yake inajipanga kutangaza hali ya dharura mapema Jumanne katika mji wa Tokyo na mingine sita. Amri hiyo itadumu kwa mwezi mmoja na inawataka watu kutotoka majumbani. Serikali pia inapanga msaada wa kiuchumi wenye thamani ya dola za Marekani trilioni 1.

Austria

Nchi moja iliyokopo mwisho wa upande wa pili wa maambukizi Austria, ambapo maafisa Jumatatu wamesema wanafikiria kuanza kusitisha amri ya watu kutotoka majumbani kwa kuruhusu maduka madogo madogo kufunguliwa wiki ijayo na maduka makubwa nchini humo kuanza kutoa huduma Mei 1. Austria imethibitisha kuwepo maambukizi ya watu 12,000.

UN

Wakati huohuo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezishauri serikali kuchukuwa hatua ya kuwahami wanawake baada ya taarifa za “kusikitisha” juu ya kuongezeka kwa vitendo vya uvunjifu wa amani dhidi yao majumbani wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.