Wanyarwanda wampongeza Kagame

Watu wakicheza ngoma ba kuimba kuunga mkono chama cha Rwandan Patriotic Front (RPF) na mgombea urais Paul Kagame . Picha na LUIS TATO / AFP

Wananchi wengi wa Rwanda wamepongeza ushindi wa kiongozi wao Paul Kagame, baadhi wakisema habidi kuondoka madarakani la sivyo nchi hiyo itatumbukia katika ghasia.

Akijitayarisha kuingia madarakani kwa mhula wa nne, baada ya kushinda asili mia 99.15 za kura kufuatana na matokeo ya awali kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 66 alisema hii leo kwamba matokeo hayo yanaonesha uwamunifu aliopewa na Wanyarwanda na sio takwimu tu kwani ni idadi kubwa mno.

Amesema anatumaini kufanya kazi pamoja kutatua matatizo yote ya nchi hiyo.

Wakazi wa Kigali katika soko la Nyabugogo waliliambia shirika la habari la AFP kwamba wameridhika na matokeo na hawamuoni mtu mwengine anayeweza kuwaunganisha pamoja, vyovote vingine wanasema kutakuwepo na mauwaji mengine.

Matokeo rasmi ya mwisho ya uchaguzi wa rais na wa bunge yatatangazwa rasmi Julai 27.