Kagame amekutana na umati wa wafuasi waliompokea kwa furaha kwenye mikutano ya kampeni ambayo inadhihirisha kutoepukika kwa ushindi wake anapowania muhula wa nne kama rais. Wakati wapinzani wake Frank Habineza wa Democratic Green Party of Rwanda na mgombea huru Philippe Mpayimana wamepata taabu kuvuta umati kwenye hafla zao.
Kagame alikabiliana na wapinzani hao hao mwaka 2017, alipopata karibu asilimia 99 ya kura. Wafuatiliaji wanasema matokeo kama hayo yanatarajiwa katika nchi ambayo upinzani mkubwa dhidi ya Kagame haujakuwepo kwa muda mrefu.
Kagame mwenye umri wa miaka 66, alichukua mamlaka kama kiongozi wa waasi waliochukua udhibiti wa serikali ya Rwanda na kumaliza mauaji ya kimbari mwaka 1994. Kagame alikuwa makamu wa rais wa Rwanda na kiongozi mkuu kutoka 1994 hadi 2000, alipokuwa rais kwa mara ya kwanza. Tangu wakati huo ametawala nchi hiyo ya Afrika Mashariki kama mtawala asiyevumilia upinzani wa kisiasa.
Forum