Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 29, 2024 Local time: 11:11

Rais Kagame wa Rwanda ametetea sifa ya kidemokrasia nchini mwake


Rais wa Rwanda, Paul Kagame
Rais wa Rwanda, Paul Kagame

Wanyarwanda milioni tisa wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi wa Julai 15 wa Rais pamoja na wabunge

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametetea sifa za kidemokrasia za nchi yake wakati kampeni zimeanza leo Jumamosi kwa ajili ya uchaguzi wa rais wa Julai 15, huku rais huyo akitarajiwa kuongeza muda wa utawala wake wa miaka 24 wenye nguvu, dhidi ya taifa hilo katika Maziwa Makuu.

Wanyarwanda milioni tisa wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi utakaofanyika sambamba na uchaguzi wa wabunge, ambao ni wa kwanza nchini humo. Kagame amekuwa kiongozi wa Rwanda tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambayo yalisababisha vifo vya watu 800,000 wengi wao wakiwa Watutsi lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Amekuwa Rais tangu mwaka 2000, kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 66 atakabiliana na wapinzani hao-hao kama walivyofanya mwaka 2017, kiongozi wa chama cha upinzani cha Democratic Green, Frank Habineza, na mwandishi wa habari wa zamani Philippe Mpayimana ambaye ni mgombea huru.

Mahakama za Rwanda zilikataa rufaa kutoka kwa viongozi maarufu wa upinzani Bernard Ntaganda na Victoire Ingabire ili kuondoa hukumu za awali ambazo ziliwazuia kugombea.

Forum

XS
SM
MD
LG