Walinzi wa Clintons, Obama wakamata vifurushi vinavyo shukiwa ni bomu

Maafisa wa polisi wakiwa mbele ya nyumba za Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton and Rais Bill Clinton katika eneo la Chappaqua, New York, Jumatano Octoba. 24, 2018.

Maafisa wa Ulinzi wa viongozi nchini Marekani wamesema wamekamata vifurushi viwili vinavyo shukiwa inawezekana “vilikuwa na mabomu,” moja kati yake kilitumwa kupitia anuani za Rais mstaafu Barack Obama na nyengine kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani Hillary Clinton, ambaye alishindwa uchaguzi mkuu baada ya Rais Donald Trump kuibuka kidedea.

Katika masaa kadhaa, Kituo cha Time Warner huko New York, ambako studio za mtandao wa habari wa CNN ziliko, wafanyakazi waliondolewa kutoka katika jengo hilo Jumatano asubuhi baada kifurushi kinachotiliwa mashaka kukutikana katika chumba ambacho barua zinahifadhiwa.

Kitu hicho kilicho kuwa katika bahasha kiliondoshwa kutoka katika eneo hilo kwa salama katika gari maalum na kikosi cha kutegua mabomu cha idara ya polisi ya mji huo.

CNN imeripoti kuwa kifurushi hicho kilikuwa kimetumwa kwa jina la Mkuu wa Idara ya Ujasusi (CIA) wa zamani John Brennan, mkosoaji wa Trump mwenye hisia za juu ambaye ni mchangiaji wa Shirika la televisheni la MSNBC, ambao ni wapinzani wa mashirika ya habari.

Maafisa wa polisi wa New York wamesema inavyo onekana ni bomu lenye uwezo wa kulipuka na kifurushi kilichokuja nalo kilikuwa na unga mweupe. Meya wa New York Bill de Blassio amesema “kile tunachokiona hapa leo ni kitendo cha kututishia” na kusisitiza kuwa hakuna vitisho vingine vilivyo thibitishwa katika jiji la New York.

Gavana wa New York Andrew Cuomo amewaambia waandishi wa habari kuwa bomu pia lilikuwa limetumwa katika ofisi yake.