Wakazi wa Khartoum wapaza sauti juu ya upungufu wa bidhaa muhimu ikiwemo dawa

Mgogoro wa Sudan.

Takriban miezi miwili ya ghasia, wakazi katika Mji mkuu Khartoum wamepaza sauti zao kuhusu kuwepo upungufu mkubwa wa bidhaa muhimu na dawa.

Wizara zote katika mji mkuu wa Sudan hazina maji safi, umeme unapatikana kwa saa chache kwa wiki, hospitali nyingi katika eneo la mapigano hazifanyi kazi na majengo ya msaada yameibiwa.

Mohamed Abdullah, mkazi wa Khartoum anasema: "Tumepitia na miezi miwili ya vita na hatujui lini vitakwisha au ni wapi vitaifikisha nchi yetu. Tunakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula katika maeneo yetu pamoja na upungufu wa dawa ya magonjwa sugu.

Anaongeza kusema: "Kuna ukosefu wa bidhaa msingi kama vile mafuta, sukari, na unga. Vitu hivi havipo na hata tukuvipata kwa bahati, kile ambacho tungenunua kwa paundi 1000 ya sudan tutapata kwa paundi 3000 na kile ambacho tungenunua kwa paundi 4000 tunanuanua kwa paundi 60,000."

Soha Abdulrahma, mkazi wa Khartoum anasema: “kiukweli tunataabika sana kutokana na vita hivi ambavyo vimeendelea kwa miezi miwili. ni miezi miwili tumekuwa katika hali mbaya na hakuna mtu aliye na uelewa isipokuwa mwenyezi Mungu, katika maeneo ya magharibi, AL junaynah , al fasil nyala. Mjini Khartoum tumezingirwa kabisa , hatuna chakula, hatujna dawa, hakuna chochote.

Mazungumzo yanayosimamiwa na Marekani na Saudi Arabia yanafanyika upande wa pili wa bahari ya Sham katika mji wa Jeddah na yanakumbwa na matatizo makubwa kuweza kupatikana ufumbuzi.

Kila mkataba umekiukwa hadi sasa licha ya kwamba pande zote mbili kusema kuwa zimeweka nia ya dhati katika mashauriano hayo n licha ya vikwazo vya Marekani.