Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:08

Mkusanyiko wa waasi kusini mwa Sudan unazusha wasi wasi wa vita kusambaa zaidi

Moshi mkubwa na moto ikiwa katika maeneo mbalimbali ya Khartoum, Sudan kufuatia mapigano kati ya wanamgambo wa RSF na majeshi ya serikali.
Moshi mkubwa na moto ikiwa katika maeneo mbalimbali ya Khartoum, Sudan kufuatia mapigano kati ya wanamgambo wa RSF na majeshi ya serikali.

Wakazi wa jimbo la Sudan Kusini la Kordofan wanaripoti kukusanyika kwa kundi kubwa la waasi hapo jana Alhamisi na hivyo kuzusha wasi wasi kwamba mapigano yanayoendelea nchini humo yanaweza kuenea hadi upande wa kusini mwa nchi.

Waasi hao ni wa kundi la SPLM –N linaloongozwa na Abdelazizi al-Hilu na wanakadiriwa kufika maelfu ya wapiganaji wenye silaha nzito nzito.

Hadi sasa haijafahamika ni upande gani al-Hilu ataelemea katika mapigano yaliyoanza katika mji mkuu wa Khartoum Aprili 15 kati ya jeshi la taifa na kikosi cha dharura cha RSF.

FILE - Aliyekuwa mgombea ugavana wa -SPLM Abdel-Aziz Adam al-Hilu akiongea na waandishi wa habari mjini Kadogli kusini mwa jimbo la Kordofan, Sudan, Mei 2, 2011.
FILE - Aliyekuwa mgombea ugavana wa -SPLM Abdel-Aziz Adam al-Hilu akiongea na waandishi wa habari mjini Kadogli kusini mwa jimbo la Kordofan, Sudan, Mei 2, 2011.

Lakini wakazi wanasema kukusanya pamoja wapiganaji wake kunazusha hofu ya kuzuka mapambano.

Wakazi hao wanasema Wapiganaji wa SPLM-N wamekusanyika katika kambi za kijeshi karibu na Kadugli, mji mkuu wa jimbo la Kordofan Kusini , na kusababisha jeshi la taifa kuimarisha vita vyake.

Na wanaongeza kusema kwamba wapiganaji wa RSF wamefunga barabara kati Kadugli na El Obeid upande wa kaskazini na kuzuia usafiri wa bidhaa.

Forum

XS
SM
MD
LG