Taarifa ya wizara ya mambo ya nje ya Sudan inajiri wiki chache baada ya kiongozi wa jeshi la Sudan Generali Abdel Fattah Burhan, kutaka Volker Parthes kuondolewa majukumu yake ya kuwa mpatanishi katika mzozo huo.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres amefamishwa kuhusu uamuzi wa serikali ya Sudan.
Tangu pril 15, jeshi la Sudan, likiongozwa na Burhan limekuwa likipigana na kikosi maalum cha jeshi cha RSF kinachoongozwa na Generali Mohmmed Hamdaan Dagalo, kila upande ukilenga kupata nguvu za kuongoza serikali.
Zaidi ya watu 860 wamefariki kutokana na vita hivyo na muungano wa madaktari nchini Sudan umesema kwamba huenda idadi ya vifo ikaongezeka.
Forum