Watu walioshuhudia wameripoti mashambulizi ya roketi mashariki mwa Khartoum na karibu na jumba la shirika la habari la serikali katika mji wa Omburdan.
Mapigano yamekuwa yakiendelea kwa karibu wiki saba, kati ya wanajeshi wa serikali na kikosi cha RSF, katika mji wa Khartoum na katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan, licha ya kuwepo juhudi zinazoendelea za Kutaka vita kusitishwa.
Jeshi la Sudan limetangaza kwamba limeongeza nguvu za wanajeshi wake mjini Khartoum kwa kuwasafirisha wanajeshi kutoka sehemu zingine za Sudan.
Marekani imewawekea vikwazo wahusika wa vita hivyo kutoka pande zote mbili kutokana na umwagikaji wa damu.
Kampuni kadhaa za silaha za jeshi la Sudan pamoja na kampuni za kuuza madini zinazodhibitiwa na kamanda wa kikosi cha RSF Mohamed Haamdan Daglo na familia yake pia zimewekewa vikwazo na Marekani.
Forum