Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:06

Mapigano yanaendelea Sudan na kusababisha vifo kwa raia


Majenerali wawili wanaohasimiana nchini Sudan, mkuu wa jeshi Jenerali Abdel fattah al-Burhan (L) na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo wa wanamgambo wa Rapid Support Forces
Majenerali wawili wanaohasimiana nchini Sudan, mkuu wa jeshi Jenerali Abdel fattah al-Burhan (L) na Jenerali Mohamed Hamdan Daglo wa wanamgambo wa Rapid Support Forces

Mapigano yameendelea katika nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika tangu kati-kati ya mwezi Aprili wakati mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza kikosi cha wanamgambo wa Rapid Support Forces walipoanza kuzozana

Waombolezaji walikusanyika kuzika maiti huku miili ya watu ikiwekwa katika hospitali moja mjini Khartoum huko Sudan siku ya Jumapili wakati mashambulizi ya makombora na risasi yalipoendelea baada ya kumalizika muda wa usitishaji mapigano uliodumu kwa saa 24 nchini Sudan.

Mapigano yameendelea katika nchi hiyo ya kaskazini mashariki mwa Afrika tangu kati-kati ya mwezi Aprili wakati mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo, ambaye anaongoza kikosi cha wanamgambo wa Rapid Support Forces walipoanza kuzozana.

Makubaliano ya karibuni ya kusitisha mapigano yaliwezesha raia waliokwama katika mji mkuu Khartoum kutoka nje na kuhifadhi akiba ya chakula pamoja na mahitaji mengine muhimu. Lakini siku ya Jumapili watu walikusanyika katika eneo la nchi kavu, kusini mwa mji mkuu wa Sudan kuwazika wahanga wa shambulizi la silaha.

Shahidi mmoja ameliambia shirika la habari la AFP kwamba dakika 10 tu baada ya kumalizika kwa mapigano hayo saa kumi na mbili asubuhi kwa saa za huko kwamba mji huo ulikumbwa tena na mashambulizi ya makombora na mapigano.

Forum

XS
SM
MD
LG