Hayo yameelezwa na maafisa wa afya wakati ghasia na vurugu kwa kiasi kikubwa zimedumaza juhudi za kuudhibiti mlipuko wa pili wa Ebola ambao umeuwa watu 2,199 tangu ulipozuka Agosti mwaka 2018.
Wanamgambo wa ndani wanaojulikana kama Mai Mai wanarudia kushambulia vituo vya afya kwa sababu wanaamini Ebola haipo na kwamba majibu yake ni njama ya kutokomeza idadi ya watu kwenye eneo hilo.
Wanamgambo wa Mai Mai mara kwa mara wanashambulia vituo vinavyotoa matibabu ya Ebola huko Mangina katika eneo la Kivu kaskazini na Byakoto huko Ituri, alisema Jean-jacques Muyembe, mkuu katika kitengo cha majibu ya Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.