Haya yamejiri wakati baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani likitarajiwa kupiga kura ya kumuondoa madarakani Rais Donald Trump wiki hii.
Kwenye barua aliomuandikia kiongozi wa walio wengi katika baraza la seneti, Mitch McConnell Jumapili amesema kuna haja ya kumuita ,mkuu wa utawala wa White House, Mick Mulvaney, msaidizi wake Robert Blair, na aliyekuwa mshauri wa usalama wa taifa, John Bolton pamoja na afisa wa bajeti Michael Duffey kutoa ushahidi.
Schumer anasema kuwa kamati inayoongoza shughuli hiyo iliomba maafisa hao kutoa ushahidi mbele yake lakini hakuna aliejitokeza.
McConnell ameashiria kufanyika kwa uamuzi wa haraka bila kuwa na shahidi yeyote akiongeza kuwa ataendelea kushirikiana na ikulu wakati akiandaa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC