Hatua hiyo imeinyima ushindi kampeni ya mrengo wa kulia kuhusu suala hilo kabla ya uchaguzi wa mwezi Juni.
Katika mfululizo wa kura 10, wanachama wa bunge la Ulaya wameidhinisha kanuni na sera ambazo zinahusu mkataba wa Uhamiaji na Hifadhi.
Mageuzi yanazungumzia suala zito la nani ana wajibu kwa wahamiaji wakati wanapowasili na iwapo nchi nyingine za EU ni vyema ziwajibike katika kusaidia.
Nchi wanachama 27 wa EU lazima hivi sasa waidhinishe mpango wa mageuzi, kuna uwezekano kura itapigwa mwishoni mwa mwezi huu, kabla ya sheria kuazna kufanya kazi.
Rais wa bunge la Ulaya, Roberta Metsola, ambaye alikuwa mbunge wa juu katika suala la uhamiaji ambaye alisaida kufungua njia kwa mpango wa mageuzi, amesema EU hivi sasa ina mfumo thabiti wa kisheria ambao “utalinda mipaka ya Ulaya.”