Rais wa Russia Vladimir Putin na rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky " wamekubali kupokea ujumbe huo na wakuu wa nchi za Afrika kote Moscow na Kyiv," Ramaphosa alisema.
Ramaphosa alisema mwishoni mwa wiki alifanya mazungumzo kwa “njia ya simu katika nyakati tofauti” na Putin na Zelensky ambapo aliwasilisha mpango ulioandaliwa na nchi za Zambia, Senegal, Jamhuri ya Congo, Uganda, Misri na Afrika Kusini.
"Nilikubaliana nao wote, Rais Putin na Rais Zelensky kuanza maandalizi ya mazungumzo na wakuu wa nchi za Afrika," Ramaphosa alisema.
"Tuna matumaini kuwa tutakuwa na majadiliano ya kina," alisema hayo wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mjini Cape Town wakati wa ziara ya kiserikali ya waziri mkuu wa Singapore Lee Hsien Loong.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Umoja wa Afrika (AU) wamefahamishwa kuhusu mpango huo na kuukubali, aliongeza Ramaphosa.
Ramaphosa hakutoa ratiba maalum au maelezo zaidi kuhusu ziara hiyo, bali alisema tu kuwa mzozo huo umekuwa "wa kuangamiza" na Afrika "pia inaathirika kwa kiasi kikubwa" kutokana vita hivyo.
Tangazo hilo limekuja siku moja baada ya Ramaphosa kusema Afrika Kusini imekuwa katika "shinikizo kubwa" kuchagua upande katika mzozo huo, kufuatia shutuka kutoka Marekani kwamba Pretoria imeipatia silaha Moscow -- hatua ambayo ingevunja msimamo wake wa kutoegemea upande wowote.
Chanzo cha habari hii nis shirika la habari la AFP.