Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:49

NATO yaionya China kuipatia silaha Russia


FILE PHOTO: Banners displaying the NATO logo are placed at the entrance of new NATO headquarters during the move to the new building
FILE PHOTO: Banners displaying the NATO logo are placed at the entrance of new NATO headquarters during the move to the new building

Wakati ulimwengu ukingoja Ukraine kuanza mashambulizi dhidi ya Russia ya majira ya machipuko, naibu katibu mkuu wa NATO, Mircea Geoana, anaionya China kutoa msaada wa kijeshi kwa Moscow huku Russia ikiendelea na uvamizi wa kikatili na kinyume cha sheria.

“Bado hatujaona dalili za China kuwasilisha silaha kuisaidia Russia, lakini tunajua majadiliano yanaendelea,” Geoana aliiambia VOA.

Alisema kwamba huu utakuwa uamuzi mzito sana wa China ambao hautaathiri tu uhusiano wao na wanachama wa NATO, lakini pia heshma yake na ulimwengu wote.

Ameongeza kusema Russia ndilo taifa chokozi katika vita na Ukraine, na kuipa Moscow silaha ni jambo tunalo laani sana.

Katika mkutano wa Pentagon Jumatatu, msemaji wa Pentagon, Brigedia Jenerali Pat Ryder aliwaambia waandishi wa habari kwamba Marekani imewasiliana na China kuhusu athari za kutoa msaada wa mauaji kwa Russia.

XS
SM
MD
LG