Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:57

Zelenskyy asema ameidhinisha mpango wa kurekebisha mifumo ya uhalifu na sheria


Volodymyr Zelenskyy
Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema katika hotuba yake ya kila siku kwa njia ya video Alhamisi, kuwa ameidhinisha mpango wa kurekebisha mifumo ya uhalifu na sheria kama sehemu ya juhudi za Ukraine kujiunga na umoja wa ulaya.

Huku ikipambana na uvamizi wa Russia, Ukraine tayari imetuma maombi ya uanachama katika jumuiya hiyo yenye mataifa wanachama 27.

Rais Zelenskyy alisema:“ Lengo letu ni kuanzisha mfumo ambao unahakikisha haki na sheria na utulivu katika nchi yetu, na pia kuzingatia lengo letu kwa Ukraine kuingia haraka katika EU. Tunaongeza utayari wetu wa kufikia lengo hili na muhimu zaidi tunahakikisha misingi ya mkataba mpya wa kijamii ambao kwa sasa unachukua sura ya kulinda taifa letu.”

Zelensky amesema mabadiliko hayo yana lengo la kuwafanya watu kujisikia salama na wanalindwa, akiongeza kuwa:“ imani ndani ya nchi inajenga uaminifu kwa wale wanaofanyakazi kwa niaba ya serikali. Polisi na mfumo wa mashtaka ni muhimu katika hili, pamoja na kila mtu mwingine anayefanyakazi ndani ya vyombo vya serikali.”

Ili kujiunga na umoja huo, ukraine ni lazima ifikie masharti kadhaa kama vile kukomesha ufisadi uliokithiri, kuimarisha sheria na kuboresha mahakama.

XS
SM
MD
LG