Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:30

Zelenskyy asema majeshi ya Russia yatatokomezwa kama Nazi ya Ujerumani ilivyoshindwa


Kutoka kushoto Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.
Kutoka kushoto Rais wa Russia Vladimir Putin na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema Jumatatu kwamba majeshi ya Russia yatatokomezwa kama Nazi ya Ujerumani ilivyotokomezwa katika Vita Vya Pili vya Dunia.

“Tulipigana wakati ule na tunapigana hivi sasa ili kusiwepo na yeyote atakayeifanya nchi nyingine kuwa watumwa na kuiharibu nchi nyingine,” Zelenskyy alisema katika ujumbe wake wa video.

“Na uovu wote ule uliopita ambao Russia ya leo inaurejesha utashindwa kama vile walivyoshindwa wenye siasa za unazi.”

Zelenskyy alisema lengo la Russia nchini Ukraine ni “kuwafanya watu watumwa au kuwaangamiza,” na alilinganisha msaada ambao Ukraine inaupata kutoka mataifa mengine na juhudi ya washirika katika kuishinda Ujerumani mwaka 1945.

“Adui huyu kwa mara nyingine ameleta uchokozi na uvamizi, kukalia kwa mabavu na kuwaondoa watu, mauaji ya watu wengi, na mateso, kupiga mabomu miji na kuchoma vijiji kinyume cha maadili yetu,” Zelenskyy alisema.

“Ushindi wetu utakuwa ni jawabu kwa yote haya. Ushindi wa Ukraine na dunia iliyo huru, ukombozi wa ardhi zetu, kurejea kwa watu wetu, kulinda maadilil yetu na, bila ya kuepukika, haki.”

Hotuba ya kiongozi wa Ukraine ilijumuisha tangazo la amri ya kiutendaji kuwepo kumbukumbu ya ushindi dhidi ya Ujerumani itakayofanyika Mei 8, kama wanavyofanya washirika wa Magharibi.

Hiyo itatofautiana na kinachofanywa na Russia, ambayo huadhimisha Mei 9.

Uvamizi wa Russia huko Crimea. Askari wenye silaha wakiwa katika Bunge la Crimea.
Uvamizi wa Russia huko Crimea. Askari wenye silaha wakiwa katika Bunge la Crimea.

Badala yake Zelenskyy alisema Ukraine itatumia Mei 9 kuenzi uungaji mkono wa Ulaya kwa Ukraine katika miaka tangu Russia ilipoikalia kimabavu Crimea na kuanzia wakati majeshi ya Russia yalipofanya uvamizi kamili mwaka jana.

XS
SM
MD
LG