Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:42

EU yapendekeza vikwazo dhidi ya kampuni za China zinazodaiwa kuuza vifaa vya kijeshi kwa Russia


Bendera za Umoja wa Ulaya zapepea nje ya makao makuu ya tume ya Umoja wa Ulaya, mjini Brussels.
Bendera za Umoja wa Ulaya zapepea nje ya makao makuu ya tume ya Umoja wa Ulaya, mjini Brussels.

Umoja wa Ulaya umependekeza vikwazo dhidi ya kampuni za China zinazotuhumiwa kuuza vifaa ambavyo vinaweza kutumiwa kama silaha kuunga mkono vita vya Russia, gazeti la Financial Times limeripoti Jumapili.

Kampuni saba za biashara za China zimeorodheshwa katika vikwazo hivyo vipya ambavyo vitajadiliwa na nchi wanachama wa EU wiki hii, ripoti hiyo imesema, ikinuku nakala ya orodha ya vikwazo ambayo gazeti la Financial Times limeiona.

Kwa mujibu wa Financial Times, orodha ya vikwazo hivyo inajumuisha kampuni mbili za China bara, 3HC Semiconductors na King-Pai Technology, pamoja na kampuni tano kutoka Hong Kong zikiwemo Sinno Electronics, Sigma Technology, Asia Pacific Links, Tordan Industry na Alpha Trading Investments.

Baadhi ya kampuni kama vile King-Pai Technology zilikuwa tayari zimechukuliwa vikwazo na Marekani, ambayo ilisema ni muuzaji mkuu kwa vitengo kadhaa katika kiwanda cha Russia cha utengenezaji wa vifaa vya kijeshi.

Tangu Russia kuanzisha uvamizi wake dhidi ya Ukraine miezi 14 iliyopita, uvamizi ambao Rais Vladimir Putin aliuita kuwa “ ni operesheni maalum ya kijeshi”, Umoja wa Ulaya umekwisha idhinisha orodha 10 za vikwazo dhidi ya watu binafsi na kampuni za Russia, na kusababisha athari za kiuchumi na kutatiza ufadhili wa vita.

XS
SM
MD
LG