Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:24

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza:Russia inakabiliwa na uhaba mbaya zaidi wa wafanyakazi katika miongo kadhaa

Wanajeshi wa Ukraine wakijiandaa kwa shambulio huko Bakhmut, mahali palipokuwa na mapigano makali zaidi na wanajeshi wa Russia, katika mkoa wa Donetsk, Ukraine, Alhamisi, Desemba 15, 2022. AP
Wanajeshi wa Ukraine wakijiandaa kwa shambulio huko Bakhmut, mahali palipokuwa na mapigano makali zaidi na wanajeshi wa Russia, katika mkoa wa Donetsk, Ukraine, Alhamisi, Desemba 15, 2022. AP

Russia inakabiliwa na uhaba mbaya zaidi wa wafanyakazi katika miongo kadhaa na vita vya Ukraine kwa kiasi fulani vinatajwa kusababisha hilo, Wizara ya Ulinzi ya Uingereza ilisema Jumapili katika taarifa za kijasusi kuhusu uvamizi wa Russia nchini Ukraine zilizoandikwa kwenye ukurasa wa Twitter.

Benki Kuu ya Russia ilifanya uchunguzi katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kugundua kuwa idadi ya watu wa Russia imepungua kwa watu milioni 2 zaidi ya ilivyotarajiwa. Hii ilitokana na vita vya Ukraine na janga la COVID ripoti hiyo ilichambua.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ilitoa madai siku ya Jumamosi kwamba Ukraine na nchi za Magharibi zinahusika na shambulizi la bomu lililotokea kwenye gari lililomjeruhi mwandishi mashuhuri wa habari wa Russia ambaye ni mzalendo na kumuua dereva wake.

Mwandishi wa Russia Zakhar Prilepin, anayejulikana kwa maoni yake ya kuunga mkono vita, alipata majeraha mabaya mguuni baada ya gari lake kulipuka siku ya Jumamosi katika eneo la Nizhny Novgorod, shirika la habari la serikali ya Russia Tass, liliripoti, likiwanukuu maafisa wa matukio ya dharura na Polisi.

XS
SM
MD
LG