Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 06:17

Mamluki wa Wagner wametishia kuondoka Bakhmut, Ukraine baada ya kupoteza wapiganaji kadhaa


Mumiliki wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin, akiwa Paraskoviivka, Ukraine. March 3, 2023. Picha: Reuters
Mumiliki wa kundi la mamluki la Wagner Yevgeny Prigozhin, akiwa Paraskoviivka, Ukraine. March 3, 2023. Picha: Reuters

Mumiliki wa kundi la mamluki la Wagner, ametishia kuondoa wapiganaji wake kutoka mji wa Bakhmut, Ukraine wiki ijayo, akishutumu jeshi la Russia kwa kukosa kupatia risasi wapiganaji wake na kupeleka kupoteza wapiganaji kadhaa.

Yevgeny Prigozhin, mfanyabiashara tahiri mwenye ushirikiano wa muda mrefu na rais wa Russia Vladimir Putin, amedai kwamba wapiganaji wa Wagner wamekuwa wamepanga kudhibithi mji wa Bakhmut ifikapo May 9, siku ambayo ni muhimu sana kwenye kalenda ya Russia kuadhimisha kushindwa kwa Kinanzi nchini Ujerumani, wakati wa vita vya pili vya dunia.

Prigozhin amesema kwamba hajapokea risasi za kutosha kutoka kwa jeshi la Russia tnagu jJumatatu.

Prigozhin anajulikana kutoa madai bila ushahidi wowote pamoja na vitisho ambavyo hatimizi.

Saa chache kabla ya kutoa taarifa yake, msemaji wake alichapisha video inyoonyesha akiwa mwenye hasira, akitaka waziri wa ulinzi wa Russia Sergei Shoigu, na mkuu wa jeshi Valery Gerasimov, kumpa risasi.

Prigozhin amekuwaa akishutumu jeshi la Russia akidai halin utaalam, tabia ambayo sio ya kawaida nchini Russia, ambayo rais Vladimir Putin ndiye mwenye uwezo pekee wa kutoa ukosoaji kama huo.

XS
SM
MD
LG