Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:47

Ramaphosa akanusha madai kwamba Afrika Kusini inaipendelea Russia


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema Jumatatu kwamba  msimamo wa nchi hiyo usiofungamana na upande wowote haupendelei Russia dhidi ya mataifa mengine na akasisitiza wito wake wa kusuluhisha mzozo wa Ukraine kwa njia ya amani.

Taarifa yake iliyotolewa katika ujumbe wa kila wiki, yalijiri baada ya madai ya Marekani wiki jana kwamba silaha zilipakiwa kwenye meli ya Kirusi Lady R, kutoka kambi ya wanamaji mjini Cape Town mwishoni mwa mwaka jana, ambayo yalizua mzozo wa kidiplomasia.

Maafisa wa Afrika Kusini walikanusha haraka madai, hayo yaliyotolewa na balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini Reuben Brigety, ambaye pia alisema maafisa wakuu wa Marekani walikuwa na "wasiwasi mkubwa" kuhusu sera ya Afrika Kusini ya kutofungamana na upande wowote, na kutoegemea upande wowote katika vita vya Russia nchini Ukraine.

"Hatukubali kwamba msimamo wetu usiofungamana na upande wowote unapendelea Russia dhidi ya nchi zingine.

Wala hatukubali kwamba msimamo huo unapaswa kuathiri uhusiano wetu na nchi zingine," Ramaphosa alisema.

Aliongeza kwamba Afrika Kusini itaendelea kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo imetia saini, na mbinu yake ya kukabiliana na madai ya Marekani ya usafirishaji wa silaha itatii makubaliano hayo.

Afisi ya Ramaphosa imesema hakuna ushahidi madhubuti uliotolewa kuunga mkono madai yaliyotolewa na balozi huyo, lakini uchunguzi utakaoongozwa na jaji mstaafu, utaangazia madai hayo.

XS
SM
MD
LG