Kutekwa kwa mji mkuu huo wa jimbo la Darfur Kusini lililopo Magharibi mwa nchi inaweza kuashiria hatua ya mabadiliko katika miezi sita ya vita vya Sudan, na yamekuja wakati pande hizo mbili zinapaswa kuanza tena mazungumzo huko Jeddah.
Jeshi halikujibu ombi la kutoa maoni, na kukatika kwa mtandao kulifanya iwe vigumu kuthibitisha dai hilo mara moja.
Wakati RSF limetawala sehemu kubwa ya ardhi ya mji mkuu wa Khartoum, jeshi limeweza kulinda kambi zake muhimu zilizoko katika mji huo.
Wakati huo huo sehemu kubwa ya serikali imehamia katika Bandari ya Sudan kwenye pwani ya Bahari ya Shamu.
RSF ilisema katika taarifa kwamba wamekamata makao makuu ya jeshi huko Nyala na kuchukua vifaa vyake vyote.
Ilichapisha kanda ya video, ambayo shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha, wakionyesha wanajeshi wake wakishangilia kwa milio ya risasi, wakidai kuwa wameiteka ngome.
Pia ilichapisha video ya kamanda wa pili wa RSF Abdelrahim Dagalo, ambaye amewekewa vikwazo na Marekani, na kusema alikuwa akiongoza juhudi hizo.
Nyala, ni kituo cha biashara ambacho waangalizi wanasema kinaweza kutumika kama ngome ya RSF, limekuwa eneo la mapigano makali, ambapo mashambulizi ya anga na mizinga limeua watu wengi, kuharibu makazi ya raia, kulemaza huduma za msingi.
RSF pia imechukua udhibiti wa Zalingei, mji mkuu wa jimbo la Kati la Darfur.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters