Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:51

Raia watatu wameuawa Sudan wakati makombora yaliposhambulia hospitali


Mfano wa maeneo yaliyoathiriwa kwa makombora nchini Sudan
Mfano wa maeneo yaliyoathiriwa kwa makombora nchini Sudan

Makombora yalianguka katika hospitali ya Al-Nau mjini Omdurman, mji pacha wa mji mkuu wa Sudan Khartoum, chanzo cha afya kimeliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu

Takriban raia watatu waliuawa siku ya Jumatatu nchini Sudan wakati makombora yaliposhambulia hospitali muhimu katika mji mkuu, chanzo cha afya kimesema wakati mapigano kati ya majenerali hasimu yakiendelea bila ya kupungua.

Makombora yalianguka katika hospitali ya Al-Nau mjini Omdurman, mji pacha wa mji mkuu wa Sudan Khartoum, chanzo cha afya kimeliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu.

Omdurman imekuwa eneo la mapigano makali kati ya jeshi la kawaida linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) vinavyoongozwa na naibu wake wa zamani Mohamed Hamdan Daglo ambaye wamekuwa vitani tangu Aprili.

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamezituhumu pande zote mbili kwa kuvilenga vituo vya afya tangu mzozo huo ulipoanza Aprili 15. Mwezi Agosti kundi la madaktari wasio na mipaka (MSF) lilionya kuwa hospitali ya Al-Nau ni moja ya vituo vya mwisho vya afya vilivyofunguliwa mjini Omdurman.

Forum

XS
SM
MD
LG