Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 05:26

Misri imewasilisha droni kwa jeshi la Sudan - Wall Street Journal


Ndege isiyo na rubani.
Ndege isiyo na rubani.

Misri imewasilisha ndege zisizo na rubani kwa jeshi la Sudan, na kuchangia uwezekano wa kuongezeka kwa mzozo ambao unaendela kuwavuta  zaidi wadau wa kikanda, Jarida la Wall Street liliripoti Jumamosi, likiwanukuu maafisa wa usalama.

Ndege zisizo na rubani za Bayraktar TB2 za Uturuki ziliwasilishwa kwa jeshi la Sudan mwezi uliopita, Jarida hilo liliripoti.

Jeshi la Sudan na kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support Service, RSF, wamekuwa kwenye mzozo wa kuwania madaraka uliozuka Aprili 15, na ambao umesababisha vifo vya mamia ya watu.

Wasemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri na jeshi la Sudan hawakujibu maombi ya kutoa kauli yaliyotumwa na gazeti hilo.

Reuters haikuweza kuthibitisha ripoti hiyo moja kwa moja.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, wiki hii limeonya kwamba dharura ya kibinadamu ya Sudan iliyochochewa na mvutano wa majenerali wawili wanaopigania udhibiti wa nchi hiyo imezua mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Mzozo huo upo ndani ya Sudan na katika nchi jirani zinazo wapa hifadhi wakimbizi, mzozo ambao una hatari wa kuyumbisha utulivu wa kanda hiyo kadiri mzozo unavyoendelea.

“Popote pale duniani ambapo mzozo unazidi kuendelea, na Sudan kuna uwezekano kuzidi kuendelea, itafanya kuwa moja ya orodha yangu ndefu ya matatizo ya muda mrefu,” alisema Ayman Gharaibeh, mkurugenzi wa ofisi ya UNHCR ya kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini.

Karibu ya watu milioni 6 nchini Sudan wamefurushwa kutoka makaazi yao toka mapigano kuanza katikati ya Aprili, na kufanya kuwa mzozo wa sasa kabisa uliosababisha wakimbizi kwa haraka zaidi duniani.

Forum

XS
SM
MD
LG